Burudani

D-Knob: Elimu imenifanya nisiwe na papara

Rapper Innocent Sahani aka D-Knob, amesema elimu aliyoipata imemfanya asiwe na papara. D-Knob ambaye wiki hii ataachia video ya wimbo wake Nishike Mkono aliomshirikisha Mwasiti ameiambia Bongo5 kuwa elimu imempa msimamo.

BgG-qhdIEAAfDT6.jpg large

“Nina uwezo wa kusema ntatoa wimbo mwezi wa saba mtu hawezi kuniyumbisha kwenye plan yangu labda kama yatokea masuala ya kiafya na nini,” amesema rapper huyo ambaye amesomea masuala ya upangaji wa miradi na kuanzisha kampuni yake ya Mitaani Most Wanted LTD.

Ameongeza kuwa tofauti na zamani, kwa sasa amekuwa na msimamo hata katika fedha anayoipokea kufanya show.

“Nimepigiwa simu nyingi lakini bado watu wanafika dau ambazo sio zangu na sio kwamba nina hela, nina njaa lakini nipo stable kwenye mind nina uwezo wa kukataa ‘kwamba usipofika hapa poa’. Elimu imenisaidia kuwa cool na kutotetereka.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents