Michezo

Dada azijibu tuhuma za Adebayor kwa familia yao ‘endelea kuidanganya dunia, hatukuhitaji tena’

Sinema ya lawama inayoendelea ndani ya familia ya mshambuliaji wa timu ya Tottenham raia wa Togo, Emmanuel Adebayor, hainoneshi kuisha mapema.

Emmanuel Adebayor

Siku mbili baada ya mshambuliaji huyo kuweka hadharani kwa post ya Facebook kuhusu mambo yanayoendelea ndani ya familia yao aliyoituhumu kwa kumchuma fedha zake na kuzitumia vibaya, mmoja wa dada zake amejibu.

ADEBAYOR AVIANIKA VISA VYA FAMILIA YAKE NA INAVYOMCHUMA FEDHA, BARUA YAKE YASIKITISHA WENGI, IMETAFSIRIWA KISWAHILI HAPA

Ni Lucia yule ambaye Adebayor kwenye post yake amemwelezea kwa kusema: Dada yangu, Lucia Adebayor huendelea kuwaambia watu kuwa baba yangu aliniambia nimlete Ulaya. Lakini nini itakuwa sababu ya kumleta Ulaya? Kila mtu yuko hapa kwa sababu.”

Lucia anasema kaka yake ni muongo mkubwa na kumkumbusha kuwa fedha si kila kitu. “Liko wapi lile gari ulilomnunulia mama.. ulilichukua,” anasema Lucia.

“Nyumba unayodai ulimnunulia dada ni uongo mtupu. Simu alizoiba Rotimi ni uongo mtupu. Pesa sio kila kitu.. sisi familia hatukuhitaji tena endelea na mambo yako na sisi tushike yetu. Kuwa nazo leo hakumaanishi kuwa utakuwa nazo kesho. Mungu akusamehe. Ulimfukuza mpwa wako saa sita usiku,” anaongeza.

“Alphas na Mallams zimekuharibia maisha yako. Unamhitaji Mungu. Ni Mungu pekee ndiye atakayeiokoa roho yako. @peace.”

Unaamini maneno ya nani?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents