Tupo Nawe

Dada wa Diamond atema nyongo Kisa Diamond “Nimeitwa Yuda sababu yake, Tumehonga media sana ili nyimbo zake zipigwe mimi na mama yangu tumetukanwa kwa sababu yake” – Video

Dada wa Diamond atema nyongo "Nimeitwa Yuda sababu ya Diamond, Tumehonga media sana ili nyimbo zake zipigwe tumetukanwa kwa sababu yake" - Video

Dada wa msanii Diamond Platnumz amefunguka mengi sana kuhusu kaka yake na kueleza kuwa kipindi Diamond hajaanzisha Tv yake alikuwa anaonewa sana na baadhi ya media “Ilifikia kipindi akitoa wimbo anatenga fungu kubwa sana la fedha ili kuhonga media zipige nyimbo zake na asipotoa hela nyimbo hazipigwi, kila media ilikuwa inakuja nyumbani inajipangia fedha na tunawapa”

Mbali na hilo Esma amefungukla jinsi Diamond alivyowagombanisha na watu na mara nyingine walikuwa wanamshauri lakini akifanya kosa anamtupia mpira yeye na kumsingizia “Kweli Diamond tulikuwa tunamshauri vitu vingi sana hasa mahusiano yake na kipindi yuko na Hamissa alikuwa akikosana nae ananisingizia mimi mpaka nikaitwa Yuda kwa sababu yake na mimi alikuwa akinisingizia siwezi kukataa, Mimi na mama yangu tumetukanwa sana kwa ajili yake, kwa ujumla tumepitia ammbo mengi sana mpaka unamuona Diamond huyu wa sasa na ninachoshukuru mungu kwa sasa amebadilika sanaa”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW