Habari

Dada wa Mariah Carey amuomba amruhusu kuwaona wapwa zake


Dada wa mwanamuziki maarufu nchini Marekani Mariah Carey, amemuomba mdogo wake huyo kumruhusu kuwaona wapwa zake kwa mara ya kwanza.

Alison Carey, aliyekuwa akijiuza kimwili ili kumsadia kumvisha na kumlisha Mariah kabla muziki haujamtoa, amemuomba Mariah kurudisha ukaribu wao ili hatimaye aweze kuwaona watoto wake mapacha Monroe (wa kike) na Moroccan Scott (wa kiume).

Mwezi uliopita mapacha hao walitimiza mwaka mmoja lakini mama yao huyo mdogo hajawahi kuwaona.

Dada hao waliokuwa karibu, walikuja kukosana mwaka 1994. Mariah na mama yao Patricia walikuwa wakigombana kumchukua ili kumlea mtoto wake wa miaka saba aitwaye Michael, wakidai kuwa alikuwa hatarini kwa kulelewa na mama mtumiaji wa madawa ya kulevya.

Alison, ambaye ni muathirika wa HIV, anakubali kuwa alifanya kazi ya uchangudoa kwenye mitaa ya New York kwa miaka mingi ambapo anasema alitumia fedha alizopata kumnunulia mdogo wake chakula na kulipa kodi ya nyumba kipindi familia yao ilipokuwa juu ya mawe.

Na sasa Alison anasisitiza kuwa amebadilika na hajatumia kilevi chochote kwa miezi minne huku akifanya kazi za ndani.

Kwa mujibu wa The Sun, juzi usiku alimwomba Mariah, 42: “Tafadhali nipigie simu.”

Akiwa mama wa watoto wanne Alison, 50, amesema: “Nataka kukutana na mdogo wangu na kumwambia ni kiasi gani nammiss na jinsi ninavyojivunia kuwa sisi ni familia moja.

“Bado nakumbuka alivyokuwa msichana mdogo, mrembo kama alivyo sasa.

“Siwezi kueleza kwa maneno jinsi nilivyofurahi kuona picha za wapwa zangu kwa mara ya kwanza. Niliona picha zao kwenye televisheni baada tu ya kuzaliwa na nimeziona nyingi zaidi walipotimiza mwaka mmoja hivi karibuni.

“Wanavutia sana. Na nikiangalia macho yao naona macho ya dada yangu yaking’aa kuniangalia— macho ambayo nilikuwa nikiyaangalia pindi nilipokuwa nikimbeba kama mtoto.

“Nina uhakika Mariah atakuja kuwa mama wa pekee na mume wake Nick Cannon, ambaye sijasikia kitu zaidi ya mazuri kumhusu, atakuwa baba mwema.

Mariah, Alison na kaka yao Morgan, 51, wamekua kwa shida kutokana na kuishi kwenye maeneo yanayokaliwa na wazungu zaidi huko Huntington, New York, ambako walinyanyasika kutokana na kuwa na mchanganyiko wa rangi.

Mara ya mwisho Alison na Mariah kuzungumza ni miaka minne iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents