Habari

DADDY DAYCARE: Mwanaume wa India mwenye familia kubwa kuliko zote duniani ‘The World’s Largest Family’, wake 39, watoto 94, wajukuu 33!!

Kama wewe ni mwanaume mwenye familia, labda ya watoto watatu na mke mmoja na huwa unalalamika maisha magumu sababu ya jukumu ulilonalo la kulea watoto na familia kwa ujumla, nina imani ukimaliza kuisoma story hii utaona aibu na kuifuta kauli hiyo na labda utasema ‘nimebarikiwa kuwa na familia ndogo’!

Kwa wale mliobahatika kupata watoto mtakubaliana namimi kuwa kulea mtoto hata mmoja ni shughuli pevu, sasa hebu ‘piga picha’ kulea watoto 30 inakuwaje? Kabla hata ‘flash’ ya picha hiyo haijawaka , hebu vuta taswira ya familia yenye jumla ya wanafamilia 181 kwenye nyumba moja, hii sio hadithi ya kutungwa shuhudia mwenyewe.

Chana-familia nzima ya watu 181
Hii ni familia nzima ya Ziona Chana yenye members 181

Idadi ya wanafamilia:

Kwanini ‘Daddy daycare’, ni zaidi ya timu ya mpira, ni zaidi ya darasa la chekechea, labda inaweza kufanana ‘kidogo’ na kituo cha kulelea watoto cha Eddie Murphy katika filamu yake ya comedy ‘DADDY DAY CARE’ iliyotoka mwaka 2003.

94+39+33+14+baba mwenye nyumba = 181. Hiyo ni idadi kamili ya wana familia ya bwana Ziona Chana kutoka India, mwanaume ambaye mwaka 2011 alifanikiwa kukaa juu ya rekodi ya dunia kwa kuwa na familia kubwa kuliko zote duniani ‘The World’s Largest Family’ kwa mujibu wa REUTERS.

Chana-akiwa na wake zake 39
Mr Chana akiwa na wake zake 39

Chana mwenye miaka 69 ndiye baba mwenye familia kubwa kuliko zote duniani, ana wake 39 (namaanisha wake wa ndoa), watoto 94 (wote damu yake), wajukuu 33 na wakwe 14 na wote wanaishi katika nyumba moja, sorry JUMBA moja (mansion).

Akiongea na The Sun baada ya kutajwa kuwa na familia kubwa kuliko zote duniani bwana Chana alisema “Today I feel like God’s special child. He’s given me so many people to look after. I consider myself a lucky man to be the husband of 39 women and head of the world’s largest family.”

Aliongeza kuwa familia imejipanga na ina nidhamu kama jeshini kila mmoja anawajibika na majukumu yake kama usafi, kufua, kupika na kadhalika.

Chana-wanawake wakiandaa mlo wa familia
Wanawake wakiandaa mlo wa familia

Chakula cha familia hiyo:

Chana alisema mlo mmoja wa jioni (dinner) kwa familia hiyo unaweza kuteketeza kuku 30, kilo 132 za viazi, kilo 220 za mchele.LOL! Hapo hatujazungumzia cha mchana wala asubuhi!

Chana-mansion kubwa kuliko zote kijijini kwao2
Jumba wanaloishi familia hiyo, ndio jumba kubwa kuliko yote kijijini kwao

Nyumba ya familia hiyo:

Familia hiyo inaishi pamoja kwenye jengo moja kubwa mithili ya hoteli lenye gharofa 4, na vyumba vipatavyo 100. Nyumba hiyo iko huko Mizoroma katika kijiji cha Baktwang, India.

Mr Chana hulala katika chumba chake mwenyewe chenye kitanda kikubwa (double), na kati ya wake zake 33, wale wadogo kiumri ndio wamepewa vyumba vya karibu na chumba chake, na wale ambao wanakaribia kuingia kijiji cha ‘mvi’ wanalala vyumba vya mbali kabisa.

Hakuna kuoneana wivu kati yao sababu kuna ratiba ya mzunguko wa yupi anayelala chumba cha ‘mfalme’ na lini hivyo kila mmoja anajua ratiba yake.

Chana- chumba kimoja wapo katika jumba hilo
Moja ya vyumba vya jumba hilo ambapo wake zake hulala kwa pamoja kama bweni la wanafunzi

Mmoja wa wake hao mwenye miaka 35 alisema ‘We stay around him as he is the most important person in the house. He is the most handsome person in the village”.

Kama vile wake alionao hawamtoshi, Mr Chana alithubutu kusema yuko radhi kwenda Marekani kutafuta wake zaidi wa kuoa sababu zoezi hilo bado linaendelea.

What a FAMILY!

SOURCE: DAILY MAIL

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents