Burudani

Dakika 45 za Young Killer kumuweka sawa Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Young Killer amesema moja ya ngoma zake alizotumia muda mfupi zaidi kuziandaa ni True Boy ambayo ilikuwa ni diss kwa Nay wa Mitego.

Rapper huyo ambaye alilazimika kufanya hivyo baada ya Nay wa Mitengo kuanza kumchana katika ngoma ‘Moto’, ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa ngoma hiyo ilichukua dakika 45 tu kuikamilisha.

“Ni verse ambayo nimeandika muda mchache, kwanza ni verse ambayo nimetumia beat ya huyo huyo Nay wa Mitego. Sijasumbuka sana kwa maana ni kitu nimeandika kama dakika 45 lakini mapokezi yalikuwa makubwa sana,” amesema Young Killer.

Alipoulizwa iwapo Nay alichukia baada ya kumchana katika ngoma hiyo, alijibu hapana kwa kueleza kuwa mwenyewe anaelewa utaratibu wa muziki wa hip hip mtu anapokuwa amekosea anawekwa sawa katika mtindo wa kumchana.

“Hapana kwa sababu yeye mwenyewe anachana watu, zile ni changamoto na inabidi ukabiliane nazo huwezi kuzikimbia , yule ni brother anaona kweli kijana kaona aniweke sawa pia muziki wetu ndio inatakiwa uwe hivyo, siyo vita, so unapoona mwenzako kakosea utamaduni wetu unaruhusu kumuweka mtu sawa kwa sababu sisi tunafanya hip hop,” amesema.

Young Killer kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Unaionaje’ ambayo amemshirikisha Harmonize.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents