Habari

Dalali: Nyumba nyingi wanazochagua wanaume, wake/wapenzi wao huzikataa!

Umeoa na unatafuta nyumba ya kupanga? Usiende kutafuta mwenyewe, kwasababu mpenzi/mke wako hatoipenda na kuna uwezekano mkubwa akaikataa.

14310682_1116692915076589_581501481_n

Kwa mujibu wa dalali maarufu jijini Dar es Salaam, Dalali Mwokozi, wanawake huzikataa nyumba zinazochaguliwa na wapenzi wao kwa kuziona mbaya.

Kinyume chake, wanaume karibu wote, huzikubali nyumba zinazochaguliwa na wapenzi wao.

Akiongea kwenye kipindi cha Brands n Cities cha Clouds TV, dalali huyo ambaye amekiri kuwa na wateja wengi wa kike, ameshauri wanaume kuwaachia wanawake wao kazi ya kutafuta nyumba kwakuwa wao ndio wanataka ziweje.

Amesema wao huangalia vigezo vingi kutokana na wengi kuwa nyumbani muda mwingi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents