Habari

Dalili ya kwamba biashara yako ina shida katika mzunguko wa fedha

Inawezekana biashara yako inaumwa kwa kipindi kirefu na ina dalili za kutokujiendesha vizuri hasa inapokuja suala la fedha za uendeshaji.

frustrated-businessman

Ila unapogundua mapema inakusaidia kufanya maamuzi sahihi na kutafuta suluhu kwa namna nyingine.  Je umeweza kukutana na dalili zifuatazo kwenye biashara yako? Angalia halafu unaweza ukafanya maamuzi;

  • Je wakati wote biashara yako inatoa hela zaidi kuliko zilizoko benki? Au unalipa zaidi kuliko kupokea?
  • Je unajikuta lazima uibane biashara yako ili ulipe mishahara kila mwezi?
  • Je biashara yako inadaiwa sana kuliko kudai? Je ulishawahi au unaendelea kuchelewesha malipo kwa wateja wako wanaokuletea mzigo?
  • Je unashindwa kulipa VAT kwa wakati? au ulishindwa kulipa kwasababu ulikuwa unaongeza mzigo wa kuuza?
  • Je unapofanyia biashara unatakiwa kulipia pango? Je mwenye eneo yuko kwenye hatua ya kukuondoa kwasababu ya wewe  kushindwa kulipa kodi kwa wakati? Kumbuka nguvu ya mwenye eneo ni kubwa kuliko ya watu wengine wanaokudai na ukiendekeza tatizo hili utaathiri biashara yako kwa kiasi kikubwa.
  • Bado unatafuta kukuza mtaji wako, ili iweze kujiendesha?
  • Je vitabu vya mahesabu vya biashara yako vinakupa ishara gani? Je madeni unayodaiwa ni mengi zaidi kuliko uwezo wa biashara? Je kuna hasara endelevu?
  • Je unahitaji kufanya kitu ili kuboresha bishara yako? bado unaona hakuna njia je umefikilia kupunguza wafanya kazi au Kuhapa eneo ulilopo kama kodi ni kubwa?
  • Kama mmiliki wa biashara je biashara yako haikusaidii kwenye maisha unayoishi kwa sababu hakuna faida?

    Kama upo kwenye jambo mojawapo hapo juu, inawezekana kwa kiasi kikubwa biashara yako inapata shida kwenye mzunguko wa fedha za kujiendesha. Suluhisho ni kwanza anza kutambua tatizo lipo na tafuta ufumbuzi wa tatizo la fedha ili kukuza au kuitoa biashara yako kwenye korongo hilo.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents