Picha

Damian Mihayo afanya ngoma na Maya Azucena wa Marekani

Aliyewahi kuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye msimu wa tano wa shindano la Tusker Project Fame, Damian Mihayo anadaiwa kufanya ngoma na mwanamuziki wa Marekani Maya Azucena aliyekuwa nchini katika ziara yake ya siku saba iliyodhaminiwa na ubalozi wa Marekani.

maya 2

Kuna uwezekano wimbo huo ukafanyika Bongo Records kwa P-Funk Majani.

Pamoja na Damian, Maya amefanya pia wimbo na kundi la Hip Hop la Masharikans la hapa nchini.

“Going 2 shoot a music video now on the streets of Dar es Salaam 4 a single I did w my TZ friends MASHARIKANS & producer Dunga,” Maya alitweet jana.

Ubalozi wa Marekani Ijumaa usiku uliandaa show maalum kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo Maya alitumbuiza akisindikizwa na wasanii wa Tanzania akiwemo Linah na wengine. Show hiyo iliyohudhuriwa na raia wengi wa kigeni ilifanyika kwenye kiota cha burudani cha Triniti kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

PICHA: MWANAMUZIKI WA MAREKANI MAYA AZUCENA ATUMBUIZA JIJINI DAR ES SALAAM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents