Burudani

Damian Soul: Nilishuhudia marafiki zangu watatu wakizama baharini na kupoteza maisha

Kila mtu ana hadithi ya kuhuzunisha katika kipindi cha maisha yake. Wengine huamua kukaa nazo mioyoni mwao, na wengine huzisema katika siku maalum. Ya Damian Soul ni kupoteza marafiki zake watatu waliozama majini akishuhudia.

13767464_1565815407048263_1458082822_n

“Mwaka 2000 nilishuhudia tukio ambalo sitolisahau maishani mwangu,” Damian ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa Jumatano hii ameandika kwenye Instagram.

“Nilipoteza marafiki zangu watatu katika tufani BAHARINI tulipokwenda kuogelea (INDIAN OCEN Mikocheni ) lililopelekea marafiki zangu hao Kuaga dunia.. na hayo yote yalitokea mbele ya macho yangu,” aliongeza.

“Ilikua ni vifo vya Uchungu nakusikitisha na Kuogopesha sana… Nilidhani nisingepona maana hakukua na msaada…lakini Kwa REHEMA ZAKE alininusuru na MAUTI.”

“MUNGU Uyo Uyo ndio Amenifikisha Hapa leo..na ndio uyu uyu amenifanya Wengi wanijue leo na kunisherekea kwa yale alionikirimia….”HAKIKA YU AISHI NDANI YANGU NI MKUU SANA” ALFA & OMEGA..hakuna Mtu wala chochote kinachoweza kuzuia Kusudi lake katika Maisha yangu. Nami ninazo kila sababu za Kumshukuru Baba Muumba maana Kusudi la mimi Kuishi linadhihirika siku hata siku kutoka Utukufu hata utukufu..nguvu moja hata nyingine…I Give THANKs 2MY HEAVENLY FATHER FOR EVERYTHING He has done in My life…. HAPPY NEW DAY to Me!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents