Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Dan Evans atangaza kurejea kwenye Tennis

Mchezaji tennis raia wa Uingereza, Dan Evans anatarajia kurejea uwanjani baada ya kutumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja kufuatia matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku michezoni.

 Mchezaji huyo aliyekuwa anashikilia nafasi ya 41, alipata fursa ya kupata mahitaji yote kutoka LTA ili aweze kurejea na sasa yupo huru kushiriki mashindano ya tennis April 24.

“Nimejifunza mengi kuhusu mimi mwenyewe kwa muda wanguI kwakuwa huu ni mchezo ninao upenda,” amesema Evans.

Hata hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ameongeza kuwa “Kwa sasa nimejiwekea muda wa kufanya mazoezi kwajuhudi kubwa na maarifa ili kuhakikisha naweza kurudi.

Dan Evans amesema kuwa kwa sasa yupo tayari kuendelea na mchezo huo baada ya kufanya mazoezi kwa juhudi kubwa licha yakuwa huwenda akachukua muda mrefu kuwa sawa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW