Habari

Daniel Craig: Skyfall premiere is the biggest and the best

Prince Charles (kulia) na mke wake Camilla (wa pili kushoto) akisalimiana na Daniel Craig wa kushoto kwenye uzinduzi wa Skyfall jijini London, Uingereza

Dar es Salaam, Kampala na Nairobi mko tayari kwa uzinduzi wa Skyfall? Kama hamko tayari basi inabidi muwe sababu yamebaki masaa tu kitu kifunguliwe toka kwenye ganda lake!

Tukupe utamu tu huu kwamba muigizaji wa sasa wa uhusika wa James Bond , Daniel Craig ametangaza kuwa uzinduzi wa filamu mpya ya Skyfall ni mkubwa zaidi kuliko 007 zote zilizopita na ambazo amezifanya yeye.

Muigizaji huyo anaecheza kama mpelelezi kwa mara ya tatu kwenye kisa hicho alikuwepo kwenye uzinduzi wa filamu hiyo katika ukumbi wa kifalme ‘Royal Albert Hall’ kuitazama filamu hiyo kwa mara ya kwanza nchini Uingereza.

“It’s incredible,” Craig aliiambia BBC. “This is my third premiere and this is the biggest and the best.”

Daniel Craig na Berenice Marlohe wakiwasili kwenye ukumbi wa Royal Albert

Skyfall is ni filamu ya 23 ya Bond huku ikiadhimisha pia miaka 50 ya kisa hicho.

Watu kibao walijitokeza kuwashangilia nyota walioigiza kwenye filamu hiyo walipokuwa kwenye red carpet maeneo ya Kensington, Magharibi mwa London.

Prince Charles na mke wake Camilla (Duchess of Cornwall) nap walikuwepo kwenye uzinduzi huo wa jana usiku.

Filamu yake ya James Bond ya mwaka 2008, Quantum of Solace iliingiza dola 586.1, na Casino Royale (2006) iliingiza milioni $594.2.

Tukutane basi kesho pale Mlimani City Cinemax Cinema kushuhudia uzinduzi wa Skyfall!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents