Tupo Nawe

Daniel Sturridge atangaza dau nono kwa atakayewezesha kupatikana kwa mbwa wake ‘Tutalipa kiasi chochote kile cha fedha’

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge ametoa ofa ya mpaka pauni 30,000 kama zawadi akirejeshewa mbwa wake.

Sturridge,29, ambaye ameondoka Liverpool mwezi uliopita baada ya mkataba wake kuisha amesema mbwa wake huyo aliibiwa baada ya wezi kuvunja nyumban yake jijini Los Angeles Marekani akiwa matembezini.

Mchezaji huyo amepakia video kwenye mtandao wake wa Instagram akionesha jinsi nyumaba yake iliyopo eneo la West Hollywood iivyoharibiwa.

“Tutalipa kiasi chochote kile ili kumpata mbwa wetu,” amesema Sturridge.

“Yoyote atakayemrudisha mbwa wangu (atapata) elfu 20, elfu 30 (pauni), kiasi chochote kile.”

Sturridge pia ametuma picha nne za mbwa huyo na pia video zinazoonesha wanaaume watatu waliojifunika uso wakiingia kwenye nyumba hiyo.

Amesema tukio hilo limetokea alipokuwa kwenye matembezi Jumatatu usiku.

Sturridge amewaambia wafuasi wake: “Yeyote anayewajua waliovunja nyumba yangu, nitakulipa utakacho. Ninamaanisha nisemacho.

“Nitatoa pesa yeyote ile – haijalishi thamani.”

Sturridge, kwa saasa anahusishwa na uhamisho kuelekea klabu ya Aston Villa ambayo inarejea EPL msimu ujao utaoanza Agosti.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW