Michezo

Daniel Sturridge atimka Liverpool

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Liverpool, Daniel Sturridge amejiunga kwa mkopo na timu ya West Brom mpaka mwisho wa msimu huu.

Sturridge amejiunga na timu hiyo baada ya kuonekana kukosa namba katika kikosi cha Liverpool tangu alipowasili kocha Jürgen Klopp mwaka 2015.

Baada ya kufanikiwa kukamilisha uhamisho wake huo wa mkopo na kukabidhiwa jezi yake yenye namba 15 ambayo amezoea kuivaa, mchezaji huyo amesema, “Nilifahamu hii itakuwa klabu sahihi kwangu. Nina marafiki hapa nilicheza nao kabla, meneja alizungumza vizuri na kuna changamoto ya timu na mtindo wa kucheza.”

Awali mchezaji huyo alikuwa anawaniwa na timu kadhaa ikiwemo Newcastle United.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents