Habari

Dar City Boyz (DCB) wanaweza kufanikiwa kama CampMulla?


Jana tumepokea wimbo mpya wa producer wa Tongwe Records, J-Ryder uitwao Tonight.

Katika wimbo huo vijana watatu wa kundi la Dar City Boyz (DCB) wameshirikishwa.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyoambatana na wimbo huo, inaonesha kuwa J-Ryder ambaye ndiye aliyeutengeneza wimbo huo yupo Vantaa, Finland.

Halafu sauti za DCB, kundi linaloundwa na vijana watatu Big Flow Santanna, Imma na Lil Harsh, zimeingizwa kwenye studio za Marshalz (India) kisha wimbo mzima kumalizikia Finland aliko ama alikokuwa J-Ryder.

Ukiusikiliza wimbo huu, ni ngumu kufikiria kuwa walioimba ni watanzania. Ni aina ya nyimbo zinazofanya vizuri sana kibiashara Ulaya na Marekani.

Nyimbo zenye mahadhi ya Electronic/Dance ni za kula bata zaidi na zinapopigwa kwenye club hakuna anayeweza kukaa.

Ni wimbo mzuri sana kwa aina hiyo ya muziki na kama ukitangazwa vizuri na tena kwa video kali yenye viwango vya video za Ulaya, J-Ryder kama producer wa wimbo huo ana nafasi ya kupata deal nyingi za kuwafanyia ngoma wasanii wakubwa kama Lady Gaga na wengine.

Nyimbo za aina hii ambazo kwa Tanzania zinaweza kuonekana ni za kawaida, ndizo zimewafikisha Campmulla (Kenya) hapo walipo leo kiasi cha kuwa nominated kwenye tuzo za BET mwaka huu.

“We have a great feeling it’s going to reach far and also taking the Tanzanian Music to the next level.” Anasema J-Ryder.

Click/fungua link hiyo hapo chini kusikiliza ama kudownload kisha tuambie unauonaje!

http://soundcloud.com/j-rydertr/tonight-j-ryder-ft-dar-city

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents