Habari

Dar es salaam haitakuwa na shida ya maji – Mh. Kamwelwe

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa uchimbaji wa visima katika eneo la Kigamboni na Temeke utakamilika mwezi Julai mwishoni huku akisema visima hivyo vitatoa lita Milioni 260 kwa siku na mwisho wa siku Dar es salaam haitakuwa na shida ya maji.

Mhe. Kamwele ameyasema hayo jana bungeni wakati akijibu swali la mbunge aliehoji;

Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni tuna mradi mkubwa sana wa maji wa visima 20 ambao ulianza mwaka 2013 na mradi huo ulikadiliwa kumalizika mwaka jana Disemba lakini haukukamilika na bahati nzuri Waziri wa Maji alitutembelea Oktoba mwaka jana na akaotoa maelezo kwa kampuni ya Serengeti kwamba ikamilishe mradi huo kabla ya Disemba mwaka jana na kama hawatafanikiwa kukamilisha watatakiwa kulipa gharama za ucheleweshaji, Je, niombe kwamba serikali itusaidie kufaham ni nini kinachendelea katika mradi ule mpaka sasa haujakamilika wakati ilikuwa suluhu la tatizo kubwa sana la maji kwa mkoa wa Dar es salaam na mkoa wa Pwani wilaya kama Mkuranga.

“Ni kweli teknolojia ya kuchimba visima imetusumbua kidogo ni visima virefu sana vinakwenda mita 400 mpaka 600 na kuna maji mengi sana kutokana na hilo ili tuwape adendamu kutokana na hiyo teknolojia kwahiyo uchimbaji wa visima utakamilika mwezi Julai mwezi ujao mwishoni,” alisema Kamwele na Kuongeza

“Visima vitakuwa vimekamilika tunatafuta fedha sasa kwaajili ya kuweka miundombinu ya usambazaji kwahiyo maeneo ya Kigamboni na Temeke yatapata maji visima hivyo vitatoa Milioni 260 kwa siku ndio maana tunasema Dar es salaam haitakuwa na shida ya maji.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents