Habari

Dar Mpya ya Makonda: Mitaa ya jiji la Dar es salaam kufungwa kamera za usalama

Katika ndoto yake ya kuendeleza falsafa ya ‘Dar Mpya’, Mkuu wa mkoa wa Jiji la Dar es salaam Paul Makonda ametangaza rasmi kuwa jiji la Dar es salaam litafungwa Kamera za ulinzi katika maeneo yote na Barabarani ili kuhakikisha matukio ya uhalifu na uvunjifu wa sheria yanatokomezwa.

RC Makonda akizungumza na wadau mbalimbali katika kikao hicho

Akielezea mango huo RC Makonda amesema kukamilika kwa mpango huo kutasaidia kupunguza uhalifu barabarani, kufichua bandari bubu, kutambua waharibifu wa barabara na mengine mengi aliyoyataja likiwemo la muda wa kufanya biashara kuongezeka kwa kile alichodai kuwa ulinzi utakuwa umeimarika.

RC Makonda ameipa siku 10 kamati atakayoiteua kutoa majibu na utaratibu mzuri kisheria kwa namna mfumo huo utakavyo fanya kazi na Idara ya Sumatra, TRA na Polisi

Katika majadaliano ya pamoja na wadau wa usalama wakiwemo Jeshi la Polisi wamefurahia mfumo huo na kuongeza kuwa  mfumo huo utasaidia zaidi na kwamba hauna budi kuanza maramoja utekelezaji wake.

Kwa mujibu wa watoa huduma hiyo (TAMOBA) wamesema mfumo huo wa Kamera pia utahusisha uangalizi wa Bodaboda, Bajaji, Daladala na magari ya serikali huku kukiwa na kituo maalumu cha ufuatiliaji, na kwamba mfumo huo utasaidia kupunguza ajali za barabarani, kusajili mabasi yaendayo mikoani, kutambua mabasi yanayokwenda kasi, ikitokea ajali trafiki watakuwa na uwezo wa kuona kwa haraka.

Uwekezaji huo unakadiriwa utagharimu kiasi cha shillingi zaidi ya bilioni 1, na utaajiri wataalamu zaidi ya 100 kwajiji la Dar es salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents