Habari

Dar: Waliodhulumiwa viwanja, nyumba, mashamba na magari waitwa na RC Makonda

Mkuu wa Mkuu wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda anawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Dar es salaam waliodhurumiwa mali zao ikiwemo Viwanja, Nyumba, Mashamba, Magari na Vifaa vingine kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala Boma kuanzia January 29 hadi February 02 kwaajili ya kupatiwa Masada wa kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, siku hiyo wamewaandalia wanasheria magwiji wa kutosha kwaajili ya kuwasikiliza, cha mihimu ni kufika na Nyaraka na vielelezo halali ili mpatiwe haki zenu.

Hii ni baada ya RC Makonda kubaini uwepo wa baadhi ya wananchi wanyonge wanaodhurumiwa na kunyanyasika kwa kuporwa haki zao na watu wenye uwezo kifedha au wanasheria wenye utaamu wanaokandamiza wennyonge.

“Serikali inayosimamiwa na Rais Magufuli ambae anamtanguliza Mungu, Mtoa haki wa kweli lazima tusimame na Mungu kuhakikisha tunasimamia haki zetu,” alisema RC Makonda kupitia taarifa hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents