Habari

Darasa kuwainua vijana zaidi ya nane kimuziki

Msanii wa Hip Hop, Darassa ameamua kuwasaidia vijana wa mtaani zaidi ya 8 wanaofanya muziki kwa kufanya nao mixtape moja itakayowatangaza nchini.

DARASA

Akizungumza na Bongo5 jana kutoka Iringa alikoenda kwenya tamasha Mitikisiko la kituo cha redio Ebony FM cha mkoani humo, Darasa alisema ameamua kuanzisha utaratibu wa kuwashirikisha vijana wa mtaani katika nyimbo zake kama njia ya kuwasaidia kuonyesha uwezo wao kwa wapenzi wa burudani.

“Mpaka sasa hivi nimeshafanya na vijana sita kutoka kutoka sehemu tofauti tofauti, bado mkoa wa Morogoro ambapo nitahitaji pia kuwapata vijana ambao tunaweza tukakamilisha mixtape,” alisema.

“Kurudisha fadhila kwa wadau wangu, ni kitu cha msingi sana,nitakuja furahi siku moja nawaona vijana ambao nimewatengeza mimi kimuziki katika game la muziki. Kwahiyo,Darassa kama Darassa ifike wakati watu waseme Darassa kafanya hili na hili huo ndiyo uzalendo na Hip Hop ya kweli.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents