Burudani

Darassa adai ukimtoa Young Killer, Stamina na Country Boy hakuna rapper mwingine aliyeng’ara

Rapper Darassa amesema kutokana na mfumo wa muziki ulivyo sasa, huenda visipatikane vipaji vipya vya wasanii wa Hip Hop nchini.

DARASA-NA-STAMINA

Akizungumza na Bongo5 leo, Darassa amesema ukiachana na yeye, Stamina, Country Boy pamoja na Young Killer hakuna kipaji kipya kichopewa nafasi ya kung’ara.

“Ninaweza sema toka tumetoka mimi, Stamina na County Boy hakuna kipaji kipya kichoibuka zaidi ya Young Killer,” amesema.

“Hakuna yeyote aliyepata nafasi na akapata benefit. Hii inasababishwa na changamoto ya muziki wa sasa kubadilika. Sasa hivi sio kipaji pekee, vinahitajika vitu vingi. Lakini tatizo kubwa naona kuna aina ya muziki umepewa kipaumbele zaidi kuliko muziki mwingine kwa imani zao.”

“Lakini mimi ninachowaambia watu waangalie muziki umebadilika zaidi hata ukiangalia wasanii wa Hip Hop kwenye show wanafanya vizuri zaidi. Kwahiyo mimi naona tunatakiwa kukuza vipaji vipya kwa sababu muziki unakua. Hatuwezi kuwa na rapper wale wale. Nafikiri kuna kitu cha kufanya kuanza kwa underground, wafanye kazi za ukweli ili hata njia ikiwa ngumu ijifungue yenyewe. Waonyeshe sababu ya kuwa wasanii.”

Katika hatua nyingine Darassa amewataka mashabiki wa muziki wake pamoja na wadau kukaa mkao wa kula kwa ujio wa kolabo mpya akiwa na Mr Blue.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents