Burudani

Darassa alikuwa aachie wimbo mpya mwezi huu lakini… – Hanscana

Mtayarishaji wa video za muziki nchini ambaye kwa sasa anafanya kazi pamoja na rapa Darassa, Hanscana, amefunguka kuzungumzia ujio mpya wa rapa huyo ambaye bado anafanya vizuri kupitia hit single yake ‘Muziki’.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Hanscana amedai Darassa alikuwa aachie wimbo mpya mwezi huu, lakini ameshindwa kutokana ratiba za show za kimataifa kumbana.

“Kusema kweli alikuwa aachie wimbo mpya mwezi huu lakini show za Rwanda na Burundi zimembana sana, amekuwa na tour ndefu sana katika nchi hizo na pia baadae ataenda nchini Kenya,” alisema Hanscana. “Tour zikiisha tu ataachia kazi mpya kwa sababu ndani tuna kazi nyingi kali, nikitendo cha kuzitoa tu,”

Hanscana amedai rapa huyo tayari ameshashoot video kadhaa za nyimbo zake ambazo hajazitoa.

Darassa amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia wimbo mpya kitendo ambacho kimewafanya mashabiki wa muziki kumsubiria kwa hamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents