Burudani

Darassa aomba radhi kwa kuchelewa kutoka kwa filamu yake ‘Sikati Tamaa’

Msanii wa Hip Hop, Darasa amewataka radhi mashabiki kwa kuchelewa kutoka kwa filamu yake ya ‘Sikati Tamaa’ na kwamba ipo tayari na itatoka.

Darasa - Mikono Juu - Sinlge Cover

Akizungumza na East Africa Radio jana, Darasa alisema filamu hiyo imechelewa kutoka kutokana na watu waliotaka kuipeleka sokoni kushindwa biashara.

“Baada ya kushindwa biashara na watu wa kwanza ambao walitaka kuipeleka filamu sokoni,kuna watu ambao wanaishughulikia hiyo filamu na makubaliano wakaniambia,’bwana una kitu kizuri zaidi cha kufanya na hiyo filamu’ nafikiri walikuwa na mipango ya kuandaa event kubwa halafu hiyo filamu izunduliwa kutokana na vitu ambavyo walinielewesha ni vitu vizuri, mimi nikawaelewa nikaona niwaachie hilo swala na jukumu lote lipo nikononi mwao,” alisema.

“Kitu ambacho nataka kuwaambia watu, mimi sio mtu wa kuamka asubuhi na kwenda kusema kitu ambacho sijui hatima yake au sitakifanya nilisema filamu itatoka, kutokana na makubaliano yetu ya mwanzo tulijua kila kitu kitakuja kuwa rahisi ,but ikaja story tofauti ambayo ikatukata ata ‘mood’ sisi. First time ya biashara watu wakatuambia wanataka kutupa kiwango cha hela ambacho hatukukubaliana nacho sisi, so haikutuingia sisi akilini ,so kitu ambacho nataka kusema kwa watu,ili sisi tupate faida,tufanye makubaliano mazuri kati yetu na watu ambao tutafanya nao biashara. Kwahiyo watu waombe Mungu tu, mimi still niko na nitafanya vitu na hiyo filamu ni kitu ambacho kimefanyika kipo na haiwezi kukaa ndani mwetu milele kitatoka, watu watusamehe kwa disappointment ambayo imetokea. Hiyo ni moja na mbili niko studio kwaajili ya kuhakikisha nafanya mambo mazuri,nataka kurudi kwenye game na watu wanisubirie,” alisema Darassa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents