Burudani

Darassa awataka wasanii kujiimarisha nyumbani kabla ya kufikiria kwenda kimataifa

Rapper Darassa amewataka wasanii kuacha kuiga njia aliyotumia Diamond Platnumz kwenda kimataifa na kuanza kwanza kujiimarisha hapa Tanzania pamoja na Afrika Mashariki.

11887103_131215600554931_1487815211_n

Darassa ameiambia Bongo5 kuwa wasanii wanatakiwa kukubalika kwanza ndani kabla ya kutaka kutoka nje.

“Kila mtu anamwona Diamond alivyopata mafanikio zaidi baada ya kufanya kolabo na Davido na akaupeleka muziki wake Nigeria,” amesema rapper huyo.

“Ni kweli hiyo kolabo imemsaidia kufika mbali zaidi, lakini Diamond tayari alikuwa ameshafanya vitu vingi nyumbani pamoja na Afrika Mashariki. Kwahiyo kwake yeye ulikuwa ni wakati sahihi ndio maana ikawa rahisi kuendelea kufanya vizuri. Lakini huwezi kufanya hivyo mtu ambaye bado haujatengeneza ramani nyumbani. Mimi kwa upande wangu, najiimarisha kwanza hapa nyumbani baadaye Afrika Mashariki halafu ndio nifikirie kutoka nje.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents