Burudani

Darassa: Pesa za show peke yake hazitoshi kuendesha maisha

Rapper Darasa amesema hawezi kutegemea mkwanja kutoka kwenye show pekee na hivyo ni ni lazima ajichanganye kwenye mishemishe mingine ili kupata mkate wake wa kila siku.

Darasa-Mikono-Juu

Akizungumza na Bongo5, DarasSa amesema mwaka 2013 umemfanya aweze kujitegemea na kuishi maisha ayatakayo huku akitegemea mishe zinazotokana na muziki.

“Nimetoa mixtape mwaka 2013 naisukuma kiaina ilimradi nipate chochote. Nimekuwa nikiprint T-shirt nakuuza. Kwahiyo mishemishe ni nyingi ambazo zinatokana na kufanya muziki. Huwezi tegemea pesa ya show ili uendeshe maisha yako inabidi ujichanganye na mishe nyingine,” amesema Darassa.

Katika hatua nyingine Darassa amesema anatarajia kutoa zawadi ya wimbo wa mapenzi kwaajili ya siku ya wapendanao ‘Valentine’s Day’ ili kuhamasisha upendo baina ya watu.

“Mwaka 2014 naanza kutoa nyimbo ya mapenzi ambayo itatoka before Valentine’s day. Itakuwa ni zawadi kwajili ya Valentine’s Day. Mashabiki wote wanaopenda muziki hii naifanya kwaajili ya kuonyema umuhimu wa upendo juu yetu ndio maana nafanya hivyo.”

“Nataka kufanya changes kidogo kwenye game yangu isiwe ile tu ambayo watu wameizoea. Kwanza nataka kutoa saluti kwa wa Bongo5, mmekuwa kila kitu kwenye muziki wetu,” ameongeza rapper huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents