Burudani ya Michezo Live

Dau la Pogba kikwazo kwa Juventus, Real Madrid, Manchester United yashikilia mpini

Manchester United kamwe hawako tayari kumuuza kiungo wao raia wa Ufaransa, Paul Pogba chini ya dau la euro milioni 100 (paundi milioni 83)

Paul Pogba will not be allowed to leave Manchester United for anything less than £83million

Kiungo huyo mtukutu anadaiwa kuhitaji kutimka Old Trafford na inatarajiwa huwenda akafanikiwa adhima yake hiyo mwishoni mwa msimu, wakati klabu za Real Madrid na Juventus zikionesha kumtolea macho.

Lakini United haipo tayari kuona inamuachia nyota wake huyo kwa dau dogo, lisilo lingana na uhalisia wa thamani ya Pogba.

Kwa mujibu wa The Guardian, United inaweza kumuachia Pogba kwa dau lenye thamani ya paundi milioni 83, lakini Juventus na Real hazipo tayari kutoa kiasi hiko cha pesa.

Hata hivyo klabu zote mbili zinadhani dau hilo ghali sana ukilinganisha na uwezo wake kwa sasa tgangu alipojiunga na United mwaka 2016.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW