Burudani

David Beckham ataka kucheza kwenye timu ya soka ya Justin Bieber



Hivi karibuni Justin Bieber alisema anataka kuanzisha timu yake ya soka na akadai atataka kocha wa timu hiyo awe David Beckham.
Hata hivyo mchezaji huyo maarufu wa soka kutoka nchini Uingereza, anataka kucheza kwenye timu hiyo na sio kuifundisha.
Alipoulizwa na mtandao wa Hollyscoop.com kama anataka kuifundisha timu hiyo, David alijibu: “Would I want to be the coach? I’d want to play!”
Hata hivyo anaweza asiruhusiwe kucheza kwenye timu hiyo kwakuwa Justin alibainisha kuwa timu yake itakuwa na maceleb wenye umri mdogo zaidi.
Wazo la Justine kuanzisha timu ya soka ni lilitokana na kuwa mpenzi wa mchezo huo na kwa miaka miwili amekuwa akicheza na kuenjoy sana.
Pamoja na kumtaka Bechham awe sehemu ya timu yake, Justin aliongeza kuwa angependa mpenzi wake Selena Gomez na mke wa David, Victoria Beckham wahusike pia kwenye mradi huo.
“I was going to ask my girl Selena and Victoria if they wanted to be cheerleaders for us. But hey, that might be pushing it.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents