Burudani

Davido aingiza mtonyo mrefu kupitia tamasha la 30 Billion

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido amedai kuingiza kiasi cha Naira Milioni 500 kupitia tamasha lake la 30 Billion Concert liliofanyika mwaka jana na amenunua dinga mpya aina ya Bentley kupitia mtonyo huo mrefu alioupata.

Tamasha hilo ambalo lilihusisha baadhi ya nchi za bara la Afrika, Ulaya na Marekani lilianza mwezi Juni mwaka uliopita na kumalizika Septemba 16 ndani ya mwaka huo limemuingiza mkali huyo pesa hiyo ndefu na kumfanya aweze kununua gari nyingine.

Kwa mujibu wa mitandao yake ya kijamii Snapchat na Instagram  hitmaker huyo wa ngoma kibao kama ‘If’ na zinginezo ameandika “On the 27TH  December me and my Team made half of Billion Facts!!”kupitia Snapchat na kwenye Instagram ameandika “🎁❤️🔥.. God you have been too good to me!! 😃,” baada ya kupost gari yake mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents