Davido amkumbuka Tagbo, kijana aliyedaiwa kumuua

Siku ya jana msanii wa muziki Davido ametumia mtandao wa kijamii wa Instagram kufanya kumbumbu ya Tagbo Umeike ambaye ni rafiki yake.

Mkali huyo ambaye kwa sasa ana tour ya ’30 Billions Africa’ ametumia mtandao huo upande wa Instastory kumkumbuka swahiba wake huyo aliyefariki Oktoba  mwaka 2017.

Kufuatia kifo cha Tagbo, Davido alijikuta katika wakati mgumu hasa pale aliptuhumiwa kupanga njama za kumuua mtu huyo kwani inadaiwa kuwa gari lilotumika kutupa mwili wa Togba lili kuwa la Davido.

Hata hivyo alijitoa katika kesi hiyo baada ya uchunguzi kubainika kuwa hakuusika licha ya kuwa mpenzi wa Tagbo ambaye ni mwanamitindo Caroline Danjuma kudai kuwa msanii huyo anahusiaka.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW