Habari

Davido apingana na Rais wa Nigeria kuelekea uchaguzi mkuu ‘hii nchi ya Demokrasia, tusikubali kuibiwa’

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido ameunga mkono juhudi za wanaharakati wanaopingana na tamko la Serikali la kutaka wananchi wa taifa hilo kurejea makwao baada ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa urais mwezi ujao.

Davido

Davido ambaye wazazi na wajomba zake wanaunga mkono chama kilichotawala muda mrefu taifa hilo cha Peoples Democratic Party (PDP) , amesema taifa hilo ni la kidemokrasia na lazima kila mtu alinde kura yake kwani ni haki yake.

Kampeni hiyo ya #Lindakurayako kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria, imeamzishwa na Chama cha PDP na ina lengo la kuzuia wizi wa kura kwenye uchaguzi mkuu mwezi Februari 16 mwaka huu.

Kama wewe ni kijana wa leo wa Nigeria. Nakushauri mwezi ujao (Februari) tuunge mkono zoezi la kupiga kura na kuzilinda. Maisha yetu ya baadae ni bora zaidi. Uchumi huu ni wa kwetu sote.” ameandika Davido kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Wikiendi iliyopita Jaji Mkuu wa Taifa hilo, alifutwa kazi na Rais Muhammadu Buhari kwa kosa la kutoa taarifa za potofu.

Taarifa hiyo, ilipelekea chama cha PDP kusimamisha kampeni zao za uchaguzi kwa masaa 72 wakidai katiba imekiukwa.

Rais wa sasa wa Nigeria, Muhammadu Buhari ndiye atakayesimama tena kwenye uchaguzi huo, kama mgombea wa Chama tawala cha APC .

Chama cha PDP, ambacho kinaungwa mkono karibia na wasanii wote wakubwa Nigeria, kimemsimamisha Makamu wa Rais wa zamani wa taifa hilo, Bilionea Atiku Abubakar ambaye alifanya kazi na Rais Oluseguni Obasanjo.

Uchaguzi wa Nigeria unakuja katika kipindi kigumu cha uchumi wa Taifa, ambalo linatajwa kuwa moja ya mataifa yaliyokithiri kwa rushwa, likishika nafasi ya 144 kati ya nchi 188. kwa mujibu wa ripoti ya T.I .

Soma zaidi – Tanzania na Rwanda zatajwa kuwa na viwango vidogo vya rushwa Afrika Mashariki, Nigeria, Kenya na Marekani ufisadi waongezeka

Chama cha PDP ndio chama pia kinachoungwa mkono na mabilionea wengi Nigeria, akiwemo baba yake Davido .

Buhari jana jumatatu akiwa katika kampeni mjini Aba, aliwataka wananchi siku ya uchaguzi wapige kura na kurudi majumbani kusubiri matokeo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents