Burudani

Davido asema collabo yake na Wizkid kutoka mwezi ujao

Hatimaye ile collabo iliyokuwa ikisubiriwa na Wanigeria na mashabiki wa muziki kote barani Afrika inakaribia kupakuliwa, ni ya mastaa ambao walikuwa hawapikiki chungu kimoja kipindi cha nyuma Davido na Wizkid.

davido n wiz

Baada ya kutoa ahadi ya kuachia collabo mpya na Diamond Platnumz mwezi ujao, Davido amesema kuwa collabo yake na Wizkid pia itatoka mwezi ujao (August).

Davido ambaye jina lake halisi ni David Adeleke, weekend iliyopita alipost picha akisheherekea tuzo ya 2015 MTV MAMA Best Male akiwa pamoja na Wizkid na kuandika: “BEST MALE 2 years in a row!! DAVIDO X WIZKID DROPS NEXT MONTH!! @wizkidayo”

Licha ya collabo hizo, album mpya ya staa huyo iitwayo ‘O.B.O’ aliyowashirikisha mastaa mbalimbali akiwemo Trey Songz, Meek Mill, Akon na wengine inatarajiwa kutoka August 10.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents