Awards

Davido ashinda tuzo ya MTV EMA kwenye kipengele cha ‘Best African Act 2017’

Msanii wa muziki  kutoka Nigeria, Davido ameshinda tuzo ya MTV EMA 2017 kwenye kipengele cha ‘Best African Act’ ambacho kilikuwa kinawaniwa na wasanii sita kutoka Afrika akiwemo hasimu wake Wizkid.

Wasanii wengine waliokuwepo kwenye kipengele hicho ni NastyC na Babes Wodumo kutoka Afrika Kusini, Nyansiski kutoka Kenya na C4 Pedro kutoka Angola.

Soma zaidi-MTV watangaza majina ya wasanii kutoka Afrika watakaowania tuzo za MTV EMA 2017

Mwaka jana tuzo hiyo ilichukuliwa na Ali Kiba kutoka Tanzania na sherehe za ugawaji wa tuzo hizo mwaka huu zinafanyika leo Novemba 12, 2017 jijini London, nchini Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents