AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Davido asitisha ghafla ziara yake ya muziki nchini Marekani, atangaza kujiunga na jeshi Nigeria (+picha)

Msanii maarufu nchini Nigeria, Davido ametangaza kusitisha ziara yake ya muziki nchini Marekani aliyooita ‘THE LOCKED UP’ na kueleza mashabiki wake kuwa ataungana na jeshi la kujenga taifa la nchi hiyo ili aingie kwenye mafunzo maalumu ya kitaifa ya National Youths Corps Services (NYCS).

Image may contain: 1 person, sitting
Davido akisaini nyaraka za kujiunga NYCS mapema mwezi Agosti mwaka huu.

 

Davido kupitia ukurasa wake wa Instagram amewaomba radhi wanaigeria wenzake na kisha kutoa tangazo la kusitisha ziara yake nchini Marekani ili kuungana na wanafunzi waliomaliza vyuo nchini humo kwenye mafunzo hayo maalumu ya kijeshi.

Mapema mwezi uliopita Davido alitangaza kuwa ataungana na Jeshi la Kujenga Taifa la nchi hiyo ili kushiriki kwa hiyari kwenye mafunzo yanayotolewa kila mwaka kwa wanafunzi wanaomaliza vyuo nchini humo.

Image may contain: 6 people, people smiling, people sitting

Davido ataungana na wanafunzi waliomaliza vyuo vikuu na vya kati nchini humo, kwenye mafunzo hayo maalumu kwa miezi mitatu Davido atakuwa akifanya mazoezi ya ukakamavu, kulima, kujenga, kufyatua tofali na shughuli nyingine kama ambavyo hapa nyumbani jeshi la JKT wanavyofanya.

Image may contain: 2 people, people standing, sky and outdoor

NYCS ni mpango wa serikali nchini Nigeria wenye lengo la kila mwanafunzi anayemaliza masomo yake ya chuo ni lazima ajiunge na Jeshi la kujenga taifa la nchi hiyo kabla ya kuajiriwa. Inaelezwa kuwa bila ya kupitia kwenye mafunzo hayo ya kijeshi basi hutaweza kuajiriwa serikalini au hata kwenye makampuni binafsi.

Image may contain: 3 people, people sitting and indoor

Hata hivyo, Davido amewatangazia mashabiki wake kuwa atatangaza baadae tarehe rasmi ya kumalizia ziara yake nchini Marekani, baada ya kumaliza mafunzo hayo.

Image may contain: 4 people, people sitting, table and indoor

Mashabiki wengi wamempongeza Davido kwa kumuita Mzalendo kwa kujitolea kuungana na wanafunzi katika shughuli za kujenga taifa hilo, huku mashabiki wake wa Marekani wamemtolea povu kwa kukatisha ziara yake.

bgarteeofficial@davidoofficial I don’t see Why you deserve to be a Nigerian copper that can stylishly and unknowingly disturb your carrer and your loving fans. Are you using NYSCE certificate to look for a job or you are satisfying your father’s Interest?. Anyway, you are a man of your own intellect and you are able to decide and define how your life would be. All i know about music is that, ‘music is jealous’…. Music doesn’t need to joke with…. take a typical lesson from #kingsunnyade ….he doesn’t joke with music at a time….. It is your fans that make people to know you as Davido…. Money cannot do everything.

queenolivianjukiYou’re trash!!!! This is the second time you flaked on your fans in LA! @davidoofficial you already lost your fan base in LA; this is not ⚾️ baseball! You don’t get three strikes! You only got two chances & you used this same bullshit excuse last year & earlier this year your dad’s private jet ran out fuel.. Those excuses work in Lagos, Nigeria!!🇳🇬🇳🇬🇳🇬 They do not work in Los Angeles, CA! 

og_saggy@davidoofficial Which duty you wan perform for NYSC baba 😅😅😅😅😅😅 na stage we need you no be for camp

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW