AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Davido awachana mashabiki wanaomtaka aachane na siasa ‘wasanii tuna nguvu, watu wanatekwa kwa kuongea ukweli’

Msanii wa muziki nchini Nigeria, Davido amewachana mashabiki wake wanaomtaka aachane na siasa kwa kuwambia kuwa yeye kama msanii ana nguvu ya kuzungumzia mambo yote yanayoonekana hayapo sawa kwenye jamii.

Related image

Davido kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema kuna watu wanamshauri asijihusishe na siasa lakini yeye amekataa kufanya akiamini kuwa ana sauti kubwa kutetea maovu kwenye jamii.


Davido ni moja ya wasanii wakubwa nchini Nigeria wanaojihusisha na siasanchinihumo, ambapo mwaka huu amejitokeza wazi wazi kumpigia upatu Mgombea Urais kwa tiketi ya PDP, Atiku Abubakar .

Sababu za kifamilia zinamfanya Davido akipigie upatu chama cha PDP, kwa sababu wazazi wake, mjomba na ndugu zake wanaunga mkono chama cha PDP na wengine wanagombea ugavana kupitia chama hicho cha Demokrasia.

Davido amekuwa mstari wa mbele kusisitiza Wanaigeria kupiga kura na kuzilinda kwenye uchaguzi mkuu Februari 16, mwaka huu.

Soma zaidi – Davido apingana na Rais wa Nigeria kuelekea uchaguzi mkuu ‘hii nchi ya Demokrasia, tusikubali kuibiwa’

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW