Burudani

Davido aweka wazi mahusiano yake na Chioma, ampa gari ya kifahari la 285m

Davido sasa ameamua kuweka wazi mahusiano yake na Chioma. Msanii huyo ameweka weka wazi hilo usiku wa jana katika sherehe ya kuzaliwa ya mrembo huyo ambaye ametimiza miaka 23.

Mara kadhaa Davido amekuwa akikataa kuwa na mahusiano na mrembo huyo. Katika sherehe hiyo Davido amemzawadia gari aina ya Porsche SUV yenye thamani ya kiasi cha dola 125k ambapo ni zaidi ya shilini milioni 285 za Kitanzania.

Lakini kubwa zaidi hit maker huyo wa Fall, kupitia Instagram, ameweka video ya gari hilo wakati akimkabidhi mrembo huyo na kuandika ujumbe wa kuthibitisha kuwa wao ni wapenzi.

“I give my baby ASSURANCE!!! I love you baby!! WE IN THIS 4 LIFE!! ❤️❤️❤️❤️😍😍😍 @thechefchi !! HAPPY BIRTHDAY CHIOM CHIOM !! FROM ME TO YOU!! I BOUGHT MY BABY A PORSCHE!! 🔥🔥🔥,” ameandika Davido.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents