Burudani

Davido aweka wazi ratiba ya ziara yake ya dunia

Davido hana masihara kwenye muziki kwa sasa. Baada ya kutikisa na wimbo wake ‘Fall’ ambao video yake imetengeneza rekodi ya kutazamwa zaidi ya mara milioni mbili katika mtandao wa YouTube ndani ya wiki moja tangu ilipoachiwa, muimbaji huyo amepanga kufanya ziara ya kimuziki.

Msanii huyo wa Nigeria ameweka wazi kufanya ziara hiyo ya dunia, ambapo atazunguka katika baadhi ya nchi za bara la Afrika, Ulaya na Marekani.

“DMW Presents : The 30 BILLION WORLD TOUR ? !! THE SUMMER IS LITT!! More dates TBA,” ameandika Davido kwenye moja a picha alizoziweka kwenye mtandao wa Instagram.

Ziara hiyo inatarajiwa kuanza Juni 23 katika mji wa Kiev nchini Ukraine na itafikia tamati nchini Guinea, Septemba 16 ya mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents