Aisee DSTV!
SwahiliFix

Davido kutumbuiza kwenye tamasha la Jay Z

Davido amepata bahati ya kutumbuiza kwenye tamasha la rapper Jay Z, ‘Made in America’.

Msanii huyo wa Nigeria atawasha moto kwenye tamasha hilo kubwa ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 1-2 mwaka huu, na kuwakutanisha zaidi ya wasanii 30 katika jukwaa moja akiwemo Nicki Minaj, Meek Mill, Fat Joe, Diplo, Miguel, Janelle Monáe, Alessia Cara, Jessie Reyez, Juice WRLD, BlocBoy JB, Saweetie na wengine.

Tamasha hilo litafanyika kwenye eneo la Benjamin Franklin Parkway, Philadelphia.

Kwa mara ya kwanza tamasha hilo lilianzishwa na Jay Z mwaka 2012, na mastaa wakubwa kama Beyonce, J cole, Cardi B, Chris Brown, Drake, 2 chainz, Kendrick Lamar wamewahi kutumbuiza.

Kwa Afrika mastaa ambao wamewahi kutumbuiza kwenye tamasha hilo ni Wizkid, Tiwa Savage, Mr Eazi na Maleek Berry.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW