BurudaniUncategorized

Davido na Young Killer kusikika kwenye ‘A Boy From Tandale’ ya Diamond

A Boy From Tandale ni moja kati ya albamu ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki.

Diamond amewataja wasanii wengine ambao watasikika kwenye albamu hiyo. Akiongea na mtangazaji wa BBC Swahili, Salim Kikeke, hitmaker huyo wa Halellujah amewataja wasanii hao kuwa ni Young Killer na Davido kutoka Nigeria.


Picha ya Diamond akiwa nchini Uingereza wiki iliyopita

“Nimewashirikisha wasanii tofauti tofauti japo kuwa wengine naogopa kuwataja ili isife. Kuna msanii kama Young Killer nimefanya nae kutoka nyumbani Tanzania, Nigeria nimefanya na Davido. Wote watakuwepo kwenye albamu yangu hii mpya ‘A Boy From Tandale’,” amesema Diamond.

Bosi huyo wa WCB ameongeza kuwa wimbo wake ambao amemshirikisha rapper Rick Rose kutoka marekani utakao toka Disemba 1 ya mwaka huu unaitwa ‘Waka’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents