Habari

Dawa ya watoto wenye baba zaidi ya mmoja yapatikana 

Kaimu Meneja wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Patricia Mputa amesema kuwa wataanza upimaji wa vinasaba (DNA) katika kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wanaodhaniwa kuwa na baba zaidi ya mmoja hayo yakijiri baada ya kuulizwa swali la kutaka kujua hatima ya watoto wanaosajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa kisha baadae inathibitika kuwa kuna baba mwingine hambaye hakutajwa kwenye cheti.

Moja ya picha inayoonyesha mashine inayotumiwa katika uchambuzi wa DNA! Hii ni mashine ya PCR.

Meneja huyo wa Rita, Patricia ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano baina ya watendaji wa Rita na viongozi wa Mkoa wa Kagera hapo jana.

Amesema utata wa nani baba halisi wa mtoto utamalizwa na vipimo vya vinasaba kwakuwa baadhi ya wanawake huandikisha majina ya baba wasiyo sahihi kwenye vyeti vya watoto.

”Kwa sababu wanazozijua wenyewe, wakati mwingine wanawake huandikisha majina ya baba mwingine ambaye si halisi kwenye cheti, lakini hilo huthibitishwa kwa DNA,’’ amesema Patricia.

Hata hivyo, Patricia ameongeza kuwa wataanza kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano mkoani Kagera kupitia ofisi za kata na vituo vya tiba huku akisistiza kutotiliwa shaka kwakuwa vitaandikwa kwa mkono.

Amesema kuwa vyeti vilivyoandikwa kwa mkono hukataliwa katika baadhi ya maeneo na baadhi ya mamlaka lakini ni halali na vinatakiwa kutambuliwa kama vile vinavyopitia kwenye mfumo wa kielektroniki.

”Utoaji wav yeti hivyo unatarajiwa kuanza Oktoba kwa Mkoa wa Kagera,’’ amesema.

Kaimu ofisa mtendaji mkuu wa Rita, Emmy Hudson amesema mpango huo utawawezesha watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kusajiliwa na kupatiwa vyeti papo hapo ambapo awali huduma hiyo ilipatikana kwenye ofisi za wakuu wa Wilaya.

”Tayari watoto milioni 2.7 wamesajiliwa na kupata vyeti kupitia mpango huu katika mikoa sita nchini na vituo vyote vya usajili vitapewa simu za kiganjani kwaajili ya kutuma taarifa za waiosajiliwa ambazo  zitaingizwa kwenye kazidata ya wakala,’’ amesema.

Chanzo Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents