Michezo

Dawa za kulevya zamponza Dan Evans

Shirikisho la kimataifa la mchezo wa tenis ‘ITF’ limemfungia mchezaji wa Uingereza, Dan Evans kwa mwaka mmoja baada ya kukutwa na kosa la kujihusisha na madawa yaliyopigwa marufuku michezoni.

Evans ambaye yupo nafasi ya pili katika viwango vya mchezo huo nchini Uingereza amekutwa na hatia baada ya vipimo alivyochukuliwa kuonyesha kwamba anatumia Cocaine huku mwenyewe akikiri kosa hilo.

Mchezaji mwenye umri wa miaka 27 ameingia katika tatizo hilo baada ya kupimwa katika michuano ya wazi ya Barcelona ‘Barcelona Open’ April 24 na kuonekana kutumia dawa hizo, na adhabu yake kuanza kutumikia taehe hiyohiyo alipogunduliwa hivyo anatarajiwa kurejea tena uwanjani April 24 mwaka 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents