Burudani

Daz Baba apanga kufungua kituo cha mafunzo ya ujasiriamali utokanao na muziki

Member wa kundi la Daz Nundaz, Daz Baba anatarajia kuanza kufanya ziara za muziki mikoani ili kukusanya pesa zitazosaidia kuanzisha kituo cha mafunzo ya ujasiriamali utokanao na muziki.

225272_215683935116267_6207504_n

Daz ameiambia Bongo5 kuwa tayari ameshapanga kuanza na mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Mbeya.

“Hii tuor ni kwaajili ya tasisi yangu Tanzania Songambele Daima Organization,” amesema. “Hii taasisi inahusu masuala ya ujasiriamali. Kikubwa tuna malengo ya kujenga center ambayo itasaidia kuelemisha na kufundisha mambo ya ujasiriamali kwenye muziki, yaani jinsi gani msanii unaweza kuitumia sanaa yako na ikakuletea manufaa kwenye maisha yako na zikawa ajira kama ajira nyingine,” ameongeza.

“Kama unavyoona mtu akishaona kile anachofanya hakimlipi, anaamua kujichanganya, sasa hii itajaribu kuwaweka watu katika njia nzuri. Kwahiyo hii tour ninayoenda kuifanya mikoani ni kwaajili ya kukusanya pesa ambazo zitaniwezesha kuandaa matamasha makubwa zaidi ili huu mradi usimame.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents