Aisee DSTV!

DC Jerry Muro aanza kwa kuwasaidia waathirika mafuriko Arumeru

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro amefanya ziara kata ya Mbuguni kata ambayo ilikumbwa na changamoto ya mafuriko mwezi wa nne mwaka huu ambapo amewatembelea wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo na kuwafariji kwa kutoka misaada mbalimbali yakiwemo magodoro,mablanketi, vifaa vya kuhifadhia maji dawa za kutibu maji na vyandarua Pamoja na vifaa vya chakula kwa kila Kaya 60 zilizoathirika.

Mh.Mkuu wa Wilaya pia ametoa msaada wa vifaa vya usafi kwa wanafunzi wa Shule ya mbugunii ukiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mh.Rais John pombe Magufuli katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata Elimu bora huku akiwa katika mazingira bora ya kusoma.

Wananchi wamemshukuru Mh Rais kwa kumteua Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ambaye tayari ameanza kuwahudumia kwa kuwaletea misaada.

Pia wananchi wamempongeza Rais Magufuli kwa kuendelea kutafuta wadau mbalimbali wa Maendeleo ambao wameanza kuunga mkono jitihada za serikali hususani katika upande wa kukabiliana na majanga kupitia kazi nzuri inayofanywa na Shirika la msalaba mwekundu Tanzania ( Tanzania RedCross )

Related Articles

4 Comments

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW