Habari

DC Jerry Muro ampa saa 48 mkuu wa TAKUKURU Arumeru 

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha Jerry Muro amempa saa arobaini na nane mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani humo za kumkamata mtu mmoja anayedaiwa kuhusika na vitendo vingi vya utapeli wa kuuza mashamba na viwanja kwa kuwagonganisha wanunuzi.

Mkuu wa wilaya huyo Jerry Muro ametoa agizo hilo wakati akikabidhi shilingi milioni 21.7 zilizookolewa na TAKUKURU wilayani humo ambazo ni za makundi mawili tofauti ya watu waliotaka kudhulumiwa ama na waajiri wao au wabia katika biashara.

Kwa upande wake mkuu wa TAKUKURU katika wilaya ya Arumeru Deo Mtui ametoa ufafanuzi wa fedha zilizookolewa ambapo shilingi milioni 14 zimetokana na deni la Emmanuel Kilembe baada ya kuuza gari kwa shilingi Milioni 23.

Ameeleza kiasi kingine cha shilingi Milioni 7.7 zimetokana na deni la mishahara ya walimu Abdallah Marambo,Ezakiel Mwaipopo,Andrew Mike,Samson Hamza,Christina Lakashu na Ellen Lomay walilokuwa wanaidai shule ya sekondari Mariado iliyopo Arumeru.

Nao waliokabidhiwa fedha zilizookolewa Abdalla Marambo na Emmanuel Kirembe wameeleza mitaani bado kuna watu wengi wanyonge ambao wamedhulumiwa na wenye uwezo na wakatoa wito wa kukimbilia TAKUKURU.

Chanzo Channel ten

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents