Habari

DC Jokate aomba Watanzania kuchangia bilioni 4.1 kutokomeza Zero Kisarawe

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Joket Mwegelo amezindua kampeni ya tokomeza ziro kwa wanafunzi wa kidato cha nne na cha sita ili wanafunzi wafaulu mitihani yao.

Akizungumza hayo leo Septemba 19, 2028 alipokuwa kwenye Shule ya Sekondari Chanzige, Jokate amesema kampeni hiyo ilizinduliwa tangu mwaka 2017 ambapo ilisaidia kuondoa ziro 455 mpaka 259.

“Ukimsaidia mtoto aweze kupata elimu unakuwa umeisaidia Tanzania nzima mfano kama mimi nimekuja hapa Kisarawe hivyo tunataka hawa wanafunzi kuanzia kidato cha nne na cha sita tufute ziro zisiwepo kabisa,” amesema Jokate.

Amesema kambi hiyo inasaidia watoto kusoma kwa makini na kuepuka vishawishi mbalimbali hivyo matumaini ya ufaulu yanakuwa makubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents