Habari

DC Kahama agawa mahindi na ndizi mbivu kwa wananchi wakiwa kwenye foleni wakisajili laini kwa alama za vidole

DC Kahama agawa mahindi na ndizi mbivu kwa wananchi wakiwa kwenye foleni wakisajili laini kwa alama za vidole

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga Anamringi Macha, amesema kuwa aliamua kugawa Mahindi pamoja na Ndizi mbivu kwa wananchi wake, waliokuwa wamepanga foleni ya kupata namba za utambulisho wa Taifa kutoka NIDA kwa lengo la kuwafundisha uvumilivu na kutokata tamaa katika zoezi hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha

Akizungumza leo Januari 20, 2020, DC Macha amesema kuwa lengo lake kuu lilikuwa ni kuwafanya wananchi watulie sehemu moja ili kufanikisha adhma yao ya kupata namba hizo kwa ajili ya kusajili laini zao za simu.

“Niliona nigawe hayo Mahindi na Ndizi kwa sababu, walikuwa na njaa na nilifanya hivyo ili watulie kusubiri huduma na mimi ilikuwa ni kama motivation kwao na kuwafanya wajisikie tuko pamoja na wajifunze kuvumilia, naamini jana kupata kile kidogo kuliwafanya wawe wavumilivu” amesema DC Macha.

Kwa mujibu wa DC Macha amesema ndani ya Wilaya yake, suala la wananchi kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya kupata kitambulisho cha Taifa, umeonesha kufana kwa zaidi ya asilimia 80.

Zoezi la usajili wa laini za simu kwa kutumia alama ya Vidole, linahitimishwa leo Januari 20, na kwa wale ambao watakuwa hawajasajili laini zao zitafungwa na kwamba pia zoezi hilo ni endelevu.

Chanzo Eatv.tv

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents