Bongo Movie

DC Kasesela awataka BongoMovie kuwekeza kama Diamond (Video)

Wasanii wa filamu nchini Tanzania, wakiongozwa na Jacob Stephan JB, Steve Nyerere, Jack Wolper, Aunt Ezekiel na wengine wengi wamewasili jana jioni Mkoani Iringa kwaajili ya tamasha la Amka Kijana litakalofanyika Jumamosi ya leo (April 14, 2018) katika Viwanja vya Mwembe Togwa.

Tamasha hilo lina lengo la kuwaelimisha vijana kuacha kukaa vijiweni na kuanza kuchangampia fursa mbalimbali ikiwemo kujiajiri kupitia vipaji vyao vya sanaa.

Akiongea na wasanii hao muda mchache baada ya kuwasili, DC wa Iringa Richard Kasesela amesema inasikitisha kuona tasnia ya filamu inashindwa kwenda mbele kwa kasi kubwa ambapo amewataka wasanii hao kuanza kujishughulisha na kazi nyingine nje ya sanaa zao ili kuwa na vyanzo vya mapato vya kutosha.

“Wasanii bila kufanya biashara lazima utayumba katika maisha yako, nyie wote hapa mnauwezo wa kuwa matajiri, ni jambo la kuamua tu nataka kufanya kitu fulani na mambo yakaenda,” alisema DC Kasesela.

Aliongeza, “mara ya kwanza nilitembelewa na Diamond hapa, nikamwambia tumia brand yako sasa kufanya biashara ili upate pesa, nimekaa muda nikasikia Diamond Karanga, juzi nimesikia ishu ya Wasafi TV haya ni mafanikio makubwa sana,”

DC huyo aliwataka wasanii hao kuwekeza mkoani Iringa kwa kununua mashamba na kupanda miti kwani biashara hiyo imewanufaisha wengi mkoani huyo.

Alimtolea mfano msaani Aslay kwamba ni mmoja kati ya wasanii ambao anawasiliana nae kwaajili ya kufanya biashara hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents