Habari

DC Kenani wa Arusha amkamata polisi mwizi wa umeme, akutwa na bangi na madumu ya gongo (Video)

Polisi Ambaye alikuwa anaiba umeme wa Tanesco Ambao alijiunganishia Kinyume na sheria na kuweka swichi Chooni ambayo ndio ilikuwa inatumika kuiba umeme huo na kupelekea kukwepa kulipa Bili ya Umeme, Pia baada ya Kumpekua katika Nyumba Yake anayoishi pamoja na Gari yake binafsi wamemkamata na Box za Viroba vya Konyagi ambavyo vilipigwa marufuku na Serikali,lakini yeye Amekuwa akivitumia kwa Kujaza katika chupa za konyagi na Kuziuza kwa wananchi katika baa yake, pia wamekamata Kete za Bangi 20 ambazo alizihifadhi vizuri katika pochi maalumu na kuzificha katika gari yake, pamoja na hayo bado Wakakamata Gongo Lita tano ambayo aliificha katika Buti la gari yake ndogo, pia askari huyo amekamatwa na Vyuma vinavyotumika katika Ujenzi wa Miradi mbalimbali vikiwa vimehifadhiwa katika Banda la Bata kiasi cha ndoo mbili, baada ya upekuzi Wakakamta Madumu ya mafuta ya diesel yaliyojaa mafuta na aliyaficha katika sebule yake.

Mkuu wa Wilaya amemwagiza OCD wa Jiji La Arusha Kumkamata Mtuhumiwa na kumfikisha katika vyombo vya Sheria ili iwe funzo kwa wengine.

Katika operation hio Mkuu wa Wilaya aliambatana na OCD wa jiji la Arusha, OCCID pamoja na meneja Wa Tanesco Mkoa wa Arusha ambaye alifika na mainjinia wa Tanesco na Kukata umeme uliokuwa umeunganishwa darini na swichi kuwekwa Chooni kinyume na utaratibu.

Vielelezo vyote vimechukuliwa na kupelekwa Kituo cha polisi.

Amesisitiza wananchi wawe wazalendo katika Nchi yao kwani wao kama Serikali hawatamvumilia mtu yeyote na watashughulika na yeyote bila kujali cheo wala nafasi ya mtu.

Amesema lazima kila mwananchi aunge mkono Jitihada za Serikali kwani kila mmoja anaona namna Mh Rais Dr. JOHN POMBE MAGUFULI anavyopambana kuijenga nchi hii kiuchumi hivyo lazima Tumuunge mkono kwa kulinda miundombinu ya Serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents