Habari

DC Kigamboni aagiza wakuu wa shule Kidete na Somangira kuvuliwa madaraka baada ya shule zao kushika mkia kidato cha 4

Kufuatia shule sita za Dar es Salaam kuwa miongoni mwa shule kumi za mwisho katika matokeo ya kidato cha nne Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Bw. Hashium Mgandilwa ameagiza wakuu wa shule mbili zilizopo kwenye manispaa hiyo za Kidete na Somangira day kuchukuliwa adhabu kali ikiwemo kuvuliwa madaraka.

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Bw. Hashium Mgandilwa

Mkuu huyo alisema hayo baada ya kuzitembelea shule hizo mbili na kufanya mazungumzo na wadau wa elimu wilayani humo.

“Nini tufanye kwa hali hii, vilivyofanya kikao cha mimi pamoja na wakuu wa shule tulikubaliana kwamba kwa mkuu wa shule yeyote atakayefelisha kupitiliza tutamvua madaraka na atabaki hapa hapa,” Mgandilwa alikiambia kituo cha runinga cha ITV. “Hayo yalikuwa makubaliano yetu na nikawatafutia waalimu,”

Aliongeza, “Najua kuna viongozi wako hapa waliangalie hilo, hatuwezi kuendelea kulifurahia hilo wakati shule imekuwa ya mwisho kitaifa,”

Hata hivyo mkuu huyo wa shule ya Kidete alidai shule yake haikuwa ya mwisho kitaifa bali ilikuwa kwenye list ya shule ya shule kumi za mwisho kitaifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents