Michezo

De Gea atawala tuzo za Man United, ampiga chini Lukaku

Usiku wa jana klabu ya Manchester United imetoa tuzo kwa wachezaji wao waliofanya vizuri katika msimu huu.

David De Gea amefanikiwa kushinda tuzo mbili ikiwemo kubwa ya mchezaji bora wa mwaka na ile ya Sir Mutt Bursy Player of The Year.

Wengine waliofanikiwa kushinda tuzo hizo ni Nemanja Matic kupitia kipengele cha goli bora la mwaka ambalo alifunga dhidi ya Crystal Palace na Michael Carric amefanikiwa kupatiwa tuzo maalum kwa kuitumikia Man United.

Kwa upande wa wachezaji chipukizi Scott McTominay ameyeshinda tuzo ya Manager’s Player of Year, tuzo ya Reserve Team Player of Year imekwenda kwa Demetri Mitche na Tahith Chong ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents