Michezo

De Gea: Nisinge penda tena kushinda tuzo ya mchezaji bora United

Kipa namba moja wa Manchester United David De Gea amekiri kuwa asingependelea tena kupigiwa kura kuwa mchezaji bora wa klabu wa mwaka kwa mara ya nne.

De Gea baada ya kujiunga na Manchester United akitokea Atletico Madrid 2011, alipata wakati mgumu kuzoea shuruba za soka la Kiingereza lakini kipa huyo nambari moja wa Hispania aliendela na kuwa moja ya makipa mahiri katika ulimwengu wa soka.

Kwasasa ana kiwango thabiti ndani ya Old Trafford kimemfanya atwae tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa klabu katika nyakati tatu tofauti – 2014, 2015 na 2016 lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 sasa amesema hataki tuzo hiyo mwaka huu.

“Ningependelea mshambuliaji au mchezaji mwingine yeyote ashinde – mtu ambaye anaiwezesha timu kucheza vizuri na kufunga magoli, kwa sababu inapendeza zaidi ikiwa hivyo kwenye timu,” alikiambia United Review.

“Nadhani mwaka huu tumeruhusu magoli machache na tumekuwa makini muda wote na kuna maelewano mazuri zaidi katika safu ya ulinzi. Katika mechi kadhaa sasa, kama mlinda mlango nachoka kiakili.

“Kiingereza changu ni kizuri sasa kuliko ilivyokuwa mwanzo. Naweza kufanya kazi vizuri kuliko awali na ninaweza kuwasiliana na kila mmoja, jambo ambalo ni muhimu sana. Nimekuwa kipa bora zaidi ya nilivyokuja. Nimeimarika zaidi kifiziki na kiakili. Najiimarisha kwa namna nyingi niwezavyo, mara zote na nimekuwa kipa mahiri zaidi sasa.”

Man United hadi sasa wameshinda mechi saba mfululizo katika michuano yote, lakini wamesalia kwenye nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents