Burudani

De Plaizir amchagua Alikiba Kwa Bongo

Msanii DePlaizer ameweka wazi kuhusiana na hisia zake za kutaka kufaya kazi na wanamuziki wa barani afrika ikiwa ni moja katika malengo yake katika kuunyanyua muziki wa kifrika duniani

De PLaizir

 

 

 

Msanii DePlaizer ameweka wazi kuhusiana na hisia zake za kutaka kufaya kazi na wanamuziki wa barani afrika ikiwa ni moja katika malengo yake katika kuunyanyua muziki wa kifrika duniani.

 

 

 

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 anayeendeleza makamuzi huko nchini Uingereza katika jiji la Manchester ameweka wazi sana kuwa anavutiwa saaaaaana na msanii Alikiba na yuko mbioni kuangalia uwezekano wa kurekodi nae wimbo wa pamoja “nadhani nitafurahi sana iwapo nitapata nafasi ya kupiga nae mkono” alisema msanii huyo alipokuwa akifanya mahojiano na Bongo5.

 

 

 

Alitaja sababu zilizopelekea yeye kuvutiwa na msanii Alikiba, ni wimbo wake wa ‘cinderela’ kuanzia sauti na melody hata mpangili wa Beat vinamfanya jamaa azidi kupagawa na msanii huyu.

 

 

 

Wimbo wa Cinderela inasemekana uko juu sana nchini Uingereza kuliko ngoma kibao za watanzania ambazo husikika.

 

 

 

Msanii Alikiba ambaye yupo nchini Uingereza kwa sasa, kwa ziara maalum ya kimuziki ambapo ameshafanya maonesho kadhaa na hivi karibuni anatarajia kurejea nchini.

 

 

 

De Plaizir nusra achanganyikiwe baada ya kusikia msanii Alikiba amekuja nchini Uingereza kwa ajili ya maoenesho “nilipata taarifa ya ujio wa Alikiba Uk kutoka kwa meneja wangu wa Tanzania Sophia Kessy ambaye alikutana na Alikiba kabla ya kuja huku na kumtaka akutane na mimi na kupanga lolote kuhusiana na kazi za kisanii na yeye hakuwa na pingamizi, sasa nachokifanya nadhani nitahakikisha namtafuta kabla hajaondoka”

 

 

 

Unaweza kuona ni jinsi gani msanii De Plaizir anavyoweza kujitanga za pande hizi za bongo na afrika kwa ujumla, jitihada za kumtafuta alikiba bado zinaendelea na akipitakana tutasikia nae upande wake una lipi kuhusiana na show yake na kolabo yake na mtu mzima De Plaizir.

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents